Imba Sali Gusa

SAUTI KWAYA

Mfumo wa Kidijitali wa Muziki wa Kwaya za Kanisa Katoliki

Kuunganisha Kwaya, Watunzi, Walimu wa Muziki na Wadau wa Muziki wa Kwaya katika jukwaa moja la kidijitali.

0Huduma Kuu
0Makundi ya Wadau
0Uwazi wa Mapato
UTANGULIZI MFUPI

Karibu Sauti Kwaya

Sauti Kwaya ni mfumo wa kidijitali ulioundwa kuhifadhi, kukuza na kuendeleza muziki wa kwaya za Kanisa Katoliki kwa kuwezesha upatikanaji wa nyimbo (Audio & Video), nota, mafunzo, matukio, huduma za kitaalamu na fursa za mapato kwa wadau wote wa muziki wa kwaya.

Kupitia Sauti Kwaya, kwaya, watunzi, waimbaji na walimu wa muziki wanaweza kushirikiana, kujifunza, kusambaza kazi zao na kunufaika kupitia ecosystem ya muziki wa kwaya.

DIRA YETU (Vision)

Kuwa jukwaa kuu la kidijitali linaloongoza katika kuhifadhi, kuunganisha na kuendeleza Muziki Mtakatifu Tanzania, na baadaye barani Afrika na duniani.

DHIMA YETU (Mission)

Kuwezesha ukuaji wa Muziki Mtakatifu kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kuunganisha wadau, kuhifadhi kazi za muziki, kutoa mafunzo, kukuza vipaji na kuunda fursa endelevu za maendeleo na mapato.

SAUTI KWAYA INAMHUDUMIA NANI?

Imejengwa kwa Ajili ya Kila Mdau wa Muziki wa Kwaya

🎶 Kwaya

  • Kusambaza nyimbo
  • Kuuza nyimbo
  • Kutangaza matukio

✍️ Watunzi

  • Kusambaza kazi zao
  • Kulinda hakimiliki
  • Fursa ya uwezeshwaji katika kazi zao za utunzi

🎤 Waimbaji

  • Kutambulika rasmi katika ecosystem ya Utume wa Uimbaji ndani ya Kanisa
  • Kujenga profile binafsi
  • Kutangaza vipaji
  • Kupata fursa mbalimbali

🎓 Walimu wa Muziki

  • Kufundisha mtandaoni
  • Kusambaza ujuzi kwa watu wengi zaidi
  • Kupata wanafunzi

❤️ Waumini na Wapenzi wa Muziki

  • Kusikiliza nyimbo
  • Kusoma tafakari
  • Kujifunza muziki
HUDUMA ZETU

Ndani ya Sauti Kwaya Utapata

🎵

Maktaba ya Nyimbo

🎼

Nota za Muziki

🛒

Marketplace

📅

Matukio

📖

Liturujia | Masomo | Tafakari

❤️

Rita Charity

KWA NINI SAUTI KWAYA?

Zaidi ya App — Ni Ecosystem Kamili ya Muziki wa Kwaya

  • Kuunganisha wadau wote wa muziki wa kwaya
  • Kuhifadhi urithi wa muziki wa kwaya
  • Kukuza vipaji
  • Kuwezesha mapato kwa wadau
  • Kupanua usambazaji wa kazi za muziki na kazi binafsi za wadau wa Utume wa Uimbaji
  • Kujenga jamii ya muziki wa kwaya yenye mshikamano
MAPATO KWA WADAU

Mfumo wa Haki kwa Kila Mchango

Mapato yanayopatikana ndani ya ecosystem ya Sauti Kwaya yatagawiwa kwa uwiano wa haki kwa makundi husika kulingana na mchango wao na sera ya malipo ya Sauti Kwaya.

Tunajenga mazingira ambapo:

Kwaya zinanufaika
Watunzi wananufaika
Waimbaji wananufaika
Walimu wa muziki wananufaika
Wadau wengine wananufaika
Soma Sera ya Mgawanyo wa Mapato →
RITA CHARITY

Muziki Unaogusa Jamii

Sehemu ya mapato na juhudi za Sauti Kwaya zinaunga mkono huduma za kijamii kupitia Rita Charity kwa kusaidia yatima, watoto wenye uhitaji na miradi ya maendeleo ya jamii.

Jiunge na Sauti Kwaya Leo

Kuwa sehemu ya jukwaa la muziki wa kwaya za Kanisa Katoliki — Imba, Sali, Gusa.