🎶 Kwaya
- Kusambaza nyimbo
- Kuuza nyimbo
- Kutangaza matukio
Imba • Sali • Gusa
Mfumo wa Kidijitali wa Muziki wa Kwaya za Kanisa Katoliki
Kuunganisha Kwaya, Watunzi, Walimu wa Muziki na Wadau wa Muziki wa Kwaya katika jukwaa moja la kidijitali.
Sauti Kwaya ni mfumo wa kidijitali ulioundwa kuhifadhi, kukuza na kuendeleza muziki wa kwaya za Kanisa Katoliki kwa kuwezesha upatikanaji wa nyimbo (Audio & Video), nota, mafunzo, matukio, huduma za kitaalamu na fursa za mapato kwa wadau wote wa muziki wa kwaya.
Kupitia Sauti Kwaya, kwaya, watunzi, waimbaji na walimu wa muziki wanaweza kushirikiana, kujifunza, kusambaza kazi zao na kunufaika kupitia ecosystem ya muziki wa kwaya.
Kuwa jukwaa kuu la kidijitali linaloongoza katika kuhifadhi, kuunganisha na kuendeleza Muziki Mtakatifu Tanzania, na baadaye barani Afrika na duniani.
Kuwezesha ukuaji wa Muziki Mtakatifu kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kuunganisha wadau, kuhifadhi kazi za muziki, kutoa mafunzo, kukuza vipaji na kuunda fursa endelevu za maendeleo na mapato.
Mapato yanayopatikana ndani ya ecosystem ya Sauti Kwaya yatagawiwa kwa uwiano wa haki kwa makundi husika kulingana na mchango wao na sera ya malipo ya Sauti Kwaya.
Tunajenga mazingira ambapo:
Sehemu ya mapato na juhudi za Sauti Kwaya zinaunga mkono huduma za kijamii kupitia Rita Charity kwa kusaidia yatima, watoto wenye uhitaji na miradi ya maendeleo ya jamii.
Kuwa sehemu ya jukwaa la muziki wa kwaya za Kanisa Katoliki — Imba, Sali, Gusa.