Sera hii inatoa mwongozo wa mgawanyo wa mapato ya Sauti Kwaya App kwa wadau mbalimbali ndani ya ekosistemu ya
Sauti Kwaya — kwa lengo la kuhakikisha kwaya, watunzi, waimbaji, walimu wa muziki na jamii (ikiwemo watoto
yatima na walio katika mazingira magumu) wananufaika moja kwa moja kupitia Muziki Mtakatifu.
UTANGULIZI
Ada ya Mwezi: Tsh 2,500
Ada ya kila mtumiaji kwa mwezi (Tsh 2,500) imegawanywa katika makundi makuu mawili — Sauti Kwaya Earnings
Categories (SKEC):
Impact Contribution Fund (ICF)
Tsh 500 / mwezi
Sehemu hii haitumiki kuendesha App — inaelekezwa moja kwa moja kwenye mifuko minne yenye athari ya
kijamii na kisanii: Rita Charity, Songwriters Support Fund, Engagement Reward Fund na Ambassador Reward Fund.
Platform Access Fee (PAF)
Tsh 2,000 / mwezi
Hii ndiyo msingi wa kugharamia uendeshaji wa mfumo na kutoa gawio kwa kwaya zinazobeba maudhui kwenye
platform.
Pamoja na SKEC, Sauti Kwaya ina kipengele cha Direct Sell — ambapo kwaya/kikundi
hupanga bei ya wimbo kwa kila Premium User; mtumiaji akilipa bei hiyo, anapata access ya wimbo husika.
MCHANGANUO WA ICF — Tsh 500
Mifuko Minne ya Kijamii na Kisanii
20%
Rita Charity Fund
Fedha zinaelekezwa moja kwa moja kwenye shughuli za kijamii kupitia Rita Charity — kusaidia yatima na
watoto wenye uhitaji. Hukusanywa kila baada ya miezi mitatu kupitia kampeni
“Twendeni, Tuwapelekee Tabasamu” ambapo wadau wanashiriki kuamua kituo cha kutembelewa.
30%
Ambassador Reward Fund (ARF)
Inawalipa Ambassadors wanaoleta watumiaji wapya kupitia Referral Code. Mfano: Ambassador anapata
30% × Tsh 500 = Tsh 150 kila mwezi kwa kila mtumiaji aliyemleta anayeendelea kulipa
subscription. Malipo hutolewa tarehe 5 ya kila mwezi (kiwango cha chini Tsh 10,000), bila ukomo wa muda.
20%
Songwriters Support Fund (SSF)
Huwathamini na kuwawezesha watunzi wa nyimbo za Kanisa. Gawio hukokotolewa kwa uwiano wa asilimia ya
downloads za nota (PDF) za kila mtunzi kwa mwezi — mfano, nota yenye 10% ya downloads zote hupata 10% ya
fedha za SSF. Mahesabu hufanyika tarehe 25, malipo tarehe ya mwisho ya mwezi.
20%
Engagement Reward Fund (ERF)
Huzitambua na kuzizawadia kwaya zinazochangia ukuaji wa Muziki Mtakatifu kupitia followers, engagement na
maudhui. Kwaya tatu bora hupokea 30% / 20% / 15%, na kwaya zinazochipukia (emerging) hupokea 20% / 10%,
huku 5% ikiwekwa kama Stabilization & Growth Reserve.
MCHANGANUO WA PAF — Tsh 2,000
Uendeshaji wa Sauti Kwaya na Gawio kwa Kwaya
45% — Uendeshaji wa Sauti Kwaya App (Tsh 900) Operations, technology, support
55% — Gawio kwa Kwaya (Tsh 1,100) Kulingana na Views, Stream Time na Downloads
Gawio la 55% kwa kwaya hukokotolewa kwa Final Weighted Score inayozingatia:
Views — uzito wa 40%
Stream Time — uzito wa 20%
Downloads — uzito wa 40%
DIRECT SELL (DiS)
Mauzo ya Moja kwa Moja ya Nyimbo
Kwaya/kikundi hupakia wimbo kwenye kipengele cha Direct Sell na kuweka bei yake. Mtumiaji analipa kabla ya
kudownload — malipo haya hayahusiani na PAF au ICF.
75% — kwa Kwaya/Kikundi ambacho ni mwanachama wa Sauti Kwaya App
65% — kwa Kwaya/Kikundi ambacho siyo mwanachama
Asilimia iliyobaki (25% / 35%) inabaki kwa Sauti Kwaya App kwa ajili ya uendeshaji na huduma za platform.
MAREKEBISHO YA SERA
Sera Inaweza Kubadilika
Sauti Kwaya ina haki ya kufanya marekebisho kulingana na ukuaji wa platform, maoni ya wadau, mabadiliko ya
mfumo wa uchumi na mahitaji ya kisheria. Marekebisho yote yatatangazwa rasmi ndani ya App.
Una Maswali Kuhusu Sera ya Mapato?
Wasiliana nasi kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi unavyoweza kunufaika kama mdau wa Sauti Kwaya.