S K SAUTI KWAYA
Kuhusu Huduma Sera ya Mapato Faragha Wasiliana
Faragha

Sera ya Faragha

Ilisasishwa: 23 Septemba 2026

Sera hii inaeleza jinsi Sauti Kwaya App na tovuti yetu vinavyokusanya, kutumia, kuhifadhi na kulinda taarifa zako binafsi unapotumia huduma zetu.

Yaliyomo
  1. Kuhusu Sera Hii
  2. Taarifa Tunazokusanya Kutoka Kwako
  3. Jinsi Tunavyotumia Taarifa Zako
  4. Tunashiriki Taarifa na Nani?
  5. Jinsi Tunavyolinda Taarifa Zako
  6. Haki Zako Kuhusu Taarifa Zako
  7. Matumizi na Watoto
  8. Sera Hii Inaweza Kubadilika
  9. Una Maswali Kuhusu Faragha Yako?

1.Kuhusu Sera Hii

Sauti Kwaya (“sisi”, “yetu”) inaheshimu faragha yako. Sera hii inaeleza jinsi tunavyokusanya, kutumia, kuhifadhi na kulinda taarifa unazotupa unapotumia Sauti Kwaya App na tovuti yetu (www.sautikwaya.co.tz). Kwa kutumia huduma zetu, unakubali masharti ya Sera hii ya Faragha.

Endapo hukubaliani na masharti ya Sera hii, tunakushauri usitumie Sauti Kwaya App au tovuti yetu.

2.Taarifa Tunazokusanya Kutoka Kwako

Taarifa za Akaunti

Jina, barua pepe, namba ya simu, nenosiri lililohifadhiwa kwa usalama, jina la kwaya/kikundi na dhima yako (mwimbaji, mtunzi, mwalimu wa muziki, n.k.).

Maudhui Unayopakia

Nyimbo (Audio & Video), nota za muziki (PDF), picha za profaili na taarifa za matukio unazopakia kwenye jukwaa.

Taarifa za Malipo

Historia ya malipo ya subscription na Direct Sell kupitia watoa huduma wa malipo ya simu (mobile money) au Google Play Billing. Hatuhifadhi namba kamili za kadi au PIN za malipo — hizi hushughulikiwa na watoa huduma wa malipo wenyewe.

Taarifa za Matumizi

Jinsi unavyotumia App — nyimbo unazosikiliza au kudownload, aina ya kifaa, mfumo wa uendeshaji, anwani ya IP, data za log na Referral Code za Ambassador ulizotumia au kutoa.

3.Jinsi Tunavyotumia Taarifa Zako

  • Kukupatia na kuboresha huduma za Sauti Kwaya App
  • Kuchakata malipo ya subscription na Direct Sell, na kukokotoa mgawanyo wa mapato (SKEC) kwa wadau
  • Kutambua na kulipa Ambassadors kupitia Referral Code
  • Kuwasiliana nawe kuhusu akaunti yako, malipo, matukio na taarifa muhimu
  • Kulinda usalama wa jukwaa na kuzuia udanganyifu au matumizi mabaya
  • Kutii wajibu wa kisheria na maombi halali ya mamlaka husika

4.Tunashiriki Taarifa na Nani?

Hatuuzi taarifa zako binafsi kwa mtu yeyote. Tunaweza kushiriki taarifa tu na:

  • Watoa huduma wa malipo (mfano mitandao ya simu, Google Play Billing) ili kukamilisha malipo yako
  • Watoa huduma wa mfumo/teknolojia (cloud hosting, uhifadhi wa data) wanaotusaidia kuendesha App
  • Mamlaka za kisheria pale inapohitajika kisheria au kulinda haki na usalama wetu
  • Wadau wengine wa Sauti Kwaya (mfano jina la kwaya au mtunzi) endapo umechagua kuonyesha taarifa hizo hadharani kwenye profaili yako

5.Jinsi Tunavyolinda Taarifa Zako

Tunatumia hatua za kiufundi na kiutawala kulinda taarifa zako dhidi ya upotevu, matumizi mabaya au ufikiaji usioidhinishwa. Hata hivyo, hakuna njia ya usambazaji wa data mtandaoni inayo uhakika wa asilimia 100. Taarifa zako zinahifadhiwa kwa muda unaohitajika kutoa huduma au kutimiza wajibu wa kisheria, kisha huondolewa au kufanywa isiyoweza kutambulika.

6.Haki Zako Kuhusu Taarifa Zako

  • Kuona na kupata nakala ya taarifa zako
  • Kusahihisha taarifa zisizo sahihi
  • Kuomba ufutwaji wa akaunti na taarifa zako, isipokuwa pale sheria inapohitaji kuhifadhiwa
  • Kujiondoa kwenye mawasiliano ya masoko wakati wowote

Wasiliana nasi kupitia info@sautikwaya.co.tz kutekeleza haki hizi.

7.Matumizi na Watoto

Sauti Kwaya App haikusudiwi kwa matumizi ya watoto walio chini ya miaka 13 bila ridhaa ya mzazi au mlezi. Endapo mzazi au mlezi anaamini mtoto wake ametupatia taarifa binafsi bila ridhaa, tafadhali wasiliana nasi ili tuweze kuchukua hatua za kufuta taarifa hizo.

8.Sera Hii Inaweza Kubadilika

Tunaweza kubadilisha Sera hii ya Faragha mara kwa mara kulingana na mahitaji ya kisheria au uboreshaji wa huduma. Mabadiliko yoyote muhimu yatatangazwa ndani ya App na tarehe ya “Ilisasishwa” juu ya ukurasa huu itabadilishwa.

9.Una Maswali Kuhusu Faragha Yako?

Wasiliana nasi kwa maswali yoyote kuhusu Sera hii ya Faragha au jinsi tunavyoshughulikia taarifa zako.

Tutumie Email Wasiliana Nasi
S K SAUTI KWAYA

Imba | Sali | Gusa

Mfumo wa Kidijitali wa Muziki wa Kwaya za Kanisa Katoliki

Mawasiliano

+255 703 785 785

info@sautikwaya.co.tz

www.sautikwaya.co.tz

Viungo

Kuhusu Sisi

Sera ya Mgawanyo wa Mapato

Sera ya Faragha

Rita Charity

© Sauti Kwaya. Haki zote zimehifadhiwa.